Kamati ya Uendeshaji na usimamizi wa Ligi ya Bodi ya Ligi Tanzania Bara imezitoza Faini Klabu za Simba na Yanga zinazoshiriki Ligi kuu ya Soka Tanzania Bara sambamba na Klabu za TMA iliyosalia Ligi ya NBC Championship na Pamba FC ambayo imepanda Ligi kuu.

Katika ufafanuzi wa taarifa ya Kamati hiyo imeeleza kuwa Klabu ya Simba imetozwa Faini ya shilingi Milion I moja na Klabu ya yanga ikitozwa Faini ya Shilingi Milioni Tano kwa kosa la kuingia kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa kupitia milango isiyo rasmi kuelekea mchezo wao wa Kariakoo Derby.

Mchezaji wa Klabu ya Simba Clatous Chama amefungiwa michezo mitatu na kutozwa faini ya shilingi Milioni moja kwa kosa la kumkanyaga kwa makusudi mchezaji Nickson Kibabage wa Klabu ya Yanga.

Klabu ya Pamba na TMA kwa upande wao zimetozwa Faini ya Shilingi Laki tano kwa kosa la kukataa kutumia vyumba maalumu kwaajili ya kubadilishia nguo vilivyoandaliwa kwenye Uwanja wa Black Rhino kuelekea mchezo wao uliopigwa Aprili 21.

You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement