KOCHA mkuu wa klabu ya Manchester City Pep Guardiola, amemkingia kifua beki wake Kyle Walker na kusisitiza kuwa ataendelea kuwa nahodha wa kikosi chake licha ya uwepo wa changamoto za maisha yake binafsi. 

Beki huyo wa kimataifa wa England ilimbidi kuomba radhi kwa familia yake mara baada ya kukiri kuwa na mchepuko, jambo ambalo lilizua utata ndani ya familia yake.

Kocha wake amesistiza kuwa anaheshimu maamuzi ya kila mchezi wake huku akikumbusha kuwa ataendelea kumlinda na kumpa heshima kama nahodha wa kikosi. 

Ikumbukwe baada ya kuondoka Ilkay Gundogan, Walker aliyeiwezesha City kutwaa mataji 14, alipigiwa kura na wachezaji wenzake kuwa sehemu ya manahodha wa kikosi hicho mwenzi August mwaka jana.

You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement