Mchezaji wa chess mwenye umri wa miaka tisa anatazamiwa kuweka historia ya kuwa mtu mwenye umri mdogo zaidi kuwahi kuiwakilisha Uingereza kimataifa katika mchezo wowote.

Bodhana Sivanandan, kutoka Harrow, kaskazini-magharibi mwa London, atajiunga na Timu ya Wanawake ya Uingereza kwenye Olympiad ya Chess huko Hungary baadaye mwaka huu.

Yeye ni mdogo kwa takriban miaka 15 kuliko mchezaji mwenzake mwenye umri mdogo zaidi, Lan Yao mwenye umri wa miaka 23.

"Niligundua jana baada ya kurejea kutoka shuleni, wakati baba yangu aliniambia," Bodhana aliambia BBC. "Nilikuwa na furaha. Natumai nitafanya vyema, na kupata tuzo nyingine."

Malcolm Pein, meneja wa timu ya chess ya Uingereza, anasema msichana huyo wa shule ndiye mwana Chess wa Uingereza wa ajabu kuwahi kutokea.

"Inafurahisha - yuko mbioni kuwa mmoja wa wachezaji bora wa Uingereza kuwahi kuonekana," alisema.

Hata hivyo babake mtoto huyo mwenye umri wa miaka tisa, Siva, anasema haelewi ni wapi bintiye alipata talanta yake.

"Mimi ni mhitimu wa uhandisi, kama vile mke wangu, lakini sijui mchezo wa chess," aliiambia BBC. "Nilijaribu michezo kadhaa ya ligi, lakini nilikuwa nikifanya vibaya sana."

Bodhana alisema, "Wakati fulani rafiki wa baba yangu alipokuwa akirejea India, alitupatia baadhi ya mifuko michache [yenye vitu]," Bodhana alisema. "Kulikuwa na ubao wa chess, na nilipendezwa na vipande hivyo nikaanza kucheza."

Anasema chess humfanya ajisikie "vizuri" na humsaidia "vitu vingine vingi kama hesabu na jinsi ya kuhesabu".

You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement