"Tunaishukuru serikali kwa matengezo makubwa ambayo imefanya kwenye Uwanja wa Mkapa. Simba pia imetoa mchango kiasi kufanikisha hili."

"Rais wa FIFA atakuwepo, Rais wa CAF atakuwepo na marais wa vyama vya soka vya maeneo mengine hivyo inahusisha vyombo vingi za serikali."

"Tunajua kutakuwa na watu mbalimbali kutoka mikoani na jana tulikuwa na mkutano na AIR TANZANIA ili kupata punguzo la bei ya tiketi kwa mashabiki wa Simba kutoka mikoani."

"Lengo letu ni uwanja kujaa watu 60,000. Tunatarajia tiketi zitauzwa kwa haraka hivyo tiketi zikitangazwa watu wanunue kwa haraka sababu tunatarajia watu wengi kutoka nje ya Dar. Tiketi za makundi zitaendelea kuwepo (Mnyama Package)."

"Kesho kuna jambo, tuliache liwe maalumu kuelekea mchezo wa African Football League na kutakuwa na matukio kila siku hadi siku ya mchezo." - CEO Imani Kajula.

You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement