Mabingwa mara tano, Ligi ya Mabingwa Afrika TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, wametoka sare ya 0-0 dhidi ya Mabingwa watetezi wa kombe hilo kutoka Misri, Al Ahly SC kwenye mechi ya mkondo wa kwanza wa Nusu Fainali ulioandaliwa Mjini Lubumbashi, DRC, Jumamosi.



Pande hizo zitakutana tena kwa mechi ya marudio katika Uwanja wa Kimataifa wa Cairo Ijumaa, 26 Aprili 2024.

Ingawa Mazembe imesikitishwa na kutotikisa wavu nyumbani, macho yote sasa ni kwa Cairo kwani pande zote bado zina matumaini ya kufika fainali.

TP Mazembe inalenga kufika fainali kwa mara ya kwanza baada ya miaka 10 tangu waliopofuzu fainali za Ligi ya Mabingwa ya Totalenergies CAF 2015.




You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement