CAVIN JOHNSON: CHIVAVIRO KLABU ALIYOPO SASA PRESHA NI TOFAUTI NA ALIPOKUWA
Kitendo cha kukasirika baada ya kutolewa kwa straika wa Kaizer Chiefs, Ranga Chivaviro kimetafsiriwa na kocha wa muda wa timu hiyo, Cavin Johnson kama nyota huyo wa zamani wa Marumo Gallants anasumbuliwa na mfadhaiko.
Chivaviro ambaye ni mmoja wa wachezaji saba waliosajiliwa na Amakhosi ameifungia timu hiyo bao moja pekee katika mechi 12 alizocheza za mashindano yote, kitendo ambacho kimemfanya awe na hasira hasa alipotolewa na Johnson katika mchezo huo dhidi ya Polokwane City licha ya ushindi wa bao 1-0, kwenye Uwanja wa Peter Mokaba, Jumamosi.
Chivaviro akiwa Marumo Gallants alifunga mabao 10 katika mechi 20 za ligi na saba kwenye Kombe la Shirikisho la CAF.
Hata hivyo, hajafanya hivyo tangu atue Chiefs na kitendo cha kutolewa hakikumfurahisha, lakini kocha Johnson alisema yote ni tabia ya mshambuliaji anapokuwa hawapati mabao na hilo lipo kichwani kwa Chivaviro na anatakiwa kukumbuka klabu aliyoko sasa presha ni tofauti na alikokuwa.
"Nitahakikisha anarudi kuwa sawa kwa sababu unajua washambuliaji walivyo," alisema Johnson na kuongeza; "Washambuliaji ni kama makipa, wana wazimu. Wakati mwingine wanakuwa na wazimu, wanataka kufunga mabao kwa sababu ndicho kinachowafanya wajisikie vizuri wanapofunga mabao. Na ndio nadhani alipaswa kufunga moja alikuwa na nafasi nzuri, aliitengeneza mwenyewe, na akaiweka kwenye mguu wake wa kushoto. "Nilidhani kama angetulia kidogo upande wa kulia wa goli ulikuwa wazi lakini alichelewa. Kama angeupiga tu ingekuwa goli.
"Haikuwa hivyo leo, pia ametoka sehemu ambako alikuwa anafunga nadhani mabao l2 au 13 msimu mmoja." Yote hayo yanatokea kwa washambuliaji, lakini kikubwa anachotakiwa kufahamu ni hachezi tena Marumo Gallants au AJ United anacheza Kaizer Chiefs, hapa presha ni kubwa.
"Mbali na kuwa nmchezaji mzuri na mtu mzuri ambaye amekuja na presha, kwa sababu kwenye kila mchezo unaocheza, beki yeyote wa kati anacheza dhidi yake hatacheza kwa asilimia 50 atacheza kwa asilimia 150, Kwa hivyo lazima uongeze uwezo wako hadi asilimia 200 na hiyo ndiyo tofauti.