Mahakama ya Usuluhishi wa Michezo ya Shirikisho la soka Duniani FIFA iitwayo CAS, imetupilia mbali ombi la dharura la Shirikisho la soka la Algeria na USM Alger la kusitisha uamuzi uliotolewa na Kamati ya rufaa ya Shirikisho la soka Afrika, Aprili 24, 2024.


Kamati ya rufaa ya Shirikisho la soka Afrika ilikuwa imeamua kwamba USM Alger ilipoteza mechi ya kwanza ya nusu fainali ya Kombe la shirikisho dhidi ya RS Berkane kwa mabao 3-0.

Timu ya USM Alger ilijiondoa kwenye mechi ya mkondo wa pili, kwa sababu walikataa kucheza mechi hiyo na Berkane, ambayo ilikuwa imevaa jezi zenye ramani ya Ufalme wa Morocco.

You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement