KESI ya muda mrefu iliyokuwa ikimhusisha mwanamichezo wa Urusi Kamila Valieva na matumizi ya dawa za kusisimua misuli, imemalizika kwa Mahakama ya Usuluhishi wa Michezo (CAS) kumkuta na hatia na kumfungia miaka minne. 

Kwa mujibu wa CAS Valieva mwenye umri wa 17, amekutwa na hatia baada ya kugundulika alitumia dawa zilizokatazwa michezoni wakati wa maandalizi ya michuano ya Olimpiki ya majira ya baridi iliyokuwa imepangwa kufanyika Beijing mwaka 2022.

Hata hivyo rungu hilo linamaanisha kuwa mwanamichezo huyo alipewa adhabu stahiki na chombo cha udhibiti wa utumizi wa dawa za kusisimua misuli duniani (WADA), baada ya uchunguzi kukamilishwa na jopo la madaktari mwaka 2021 kabla ya michuano ya Olimpiki.

You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement