Shirikisho la riadha nchini Kenya linasema kuwa linawasiliana na serikali ya Cameroon na mamlaka ya riadha baada ya mwanariadha wa Kenya kufariki katika nchi hiyo ya Afrika Magharibi.

Charles Kipkorir Kipsang alianguka na kufariki siku ya Jumamosi baada ya kuvuka mstari wa kumalizia mbio za Mbio za Matumaini za Mlima Cameroon, zilizofanyika katika mji wa Buea, mji mkuu wa eneo la Kusini Magharibi mwa Cameroon.

Kipsang, 33, alikuwa akiongoza mbio hizo lakini alisimama kwa muda karibu na mstari wa kumaliza, gavana wa eneo hilo Bernard Okalai Bilia alinukuliwa na shirika la habari la Xinhua.

Hatimaye alivuka mstari wa kumalizia, lakini alianguka na kufa muda mfupi baadaye. "Hatuwezi kusema ni nini hasa kilifanyika.Alikuwa sawa. Alikuwa sawa baada ya mbio. Tunadhani ni kitu kama mshtuko wa moyo," Bw Bilia alinukuliwa na Xinhua.

"Tutawafahamisha kuhusu hatua zinazofuata," shirikisho la riadha nchini Kenya ilichapisha kwenye X, iliyokuwa Twitter, siku ya Jumapili.

Mbio za Matumaini za Mlima Cameroon zinafanyika kila mwaka kwenye miteremko ya Mlima Cameroon.

Inajulikana kuwa ngumu kwa sababu ya mwinuko wa eneo la mlima.

You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement