Leo jumanne majira ya Saa 1 usiku kutakua na Derby namba moja barani Afrika yaani Al ahly Cairo vs Zamarek Cairo ambapo utakua ni miongoni mwa kipolo ambacho Al ahly Cairo wanacho katika muendelezo wa ligi ya EPL (Egypt Premier league)

SASA taarifa zinaeleza kua TIMU ya Zamarek Cairo itagomee kucheza mchezo huu kwa sababu wakidai kua Wao kama Zamarek Cairo wanataka Al ahly wacheze kwanza viporo vyao vyote ndipo wao wakutane

Sasa Al ahly wapo nafasi ya 2 wakiwa wamecheza mechi 18 na alama 42 tofauti na kinara pyramid ambae amecheza mechi 25 na alama 62 sasa utofauti wa mechi ni 7 na kinara lakini utofauti wa mechi kati ya Zamarek Cairo na Al ahly Cairo ni 2 tuu

SASA Mchezo huu inabidi ufanyike leo ambapo shirikisho la mpira Misri limeridhia waamuzi kutoka Hispania ambapo mwamuzi wa kati atakua ni Alejandro Muniz Ruiz ili kuweza kutoa maamuzi sahihi 

Kumbuka mchezo huu utaenda kutoa mwanga wa nani atakua bingwa msimu huu kwani timu ya Pyramid ambao wanaongoza ligi hiyo hivyo kama Al ahly Cairo wakitoa sare au kupoteza basi pyramid watakua na nafasi kubwa kumvua ubingwa Al ahly Cairo

You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement