Kuelekea michezo ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika ambapo Simba na Yanga zitakuwa na kibarua kizito kwenye uwanja wa nyumbani, Rais wa TFF, Wallace Karia amezitembelea klabu hizo katika mazoezi yao kuwapa morali wachezaji katika michezo hiyo.

Jumatano kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa aliitembelea Simba na Alhamisi ameitembelea Yanga ikifanya mazoezi kambini Avic Town, Kigamboni.

Machi 29, 2024 Simba itacheza mchezo wa kwanza wa robo fainali ya CAFCL dhidi ya Al Ahly, huku Yanga Machi 30 ikiwa na kibarua dhidi ya Mamelodi Sundowns michezo yote ikichezwa kuanzia saa 3 usiku Kwa Mkapa.



You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement