CAFCC: KLABU YA RIVERS UNITED HAIJAPOTEZA MCHEZO WOWOTE WA NYUMBANI KOMBE LA SHIRIKISHO AFRIKA
Bingwa mtetezi wa Kombe la Shirikisho Afrika, USM Alger amepokea kichapo cha bao 1-0 kutoka kwa Rivers United kawenye Uwanja wa Kimataifa wa Godswill Akpabio, Nigeria.
Bao la Augustine Okejepha la dakika ya 10 lilitosha kuitangulizia mguu mmoja kwenye nusu fainali ya michuano hiyo huku ikisikilizia mchezo wa marudiano utakaopigwa Aprili 8, 2024 ugenini Algeria.
Rivers United tangu katika hatua ya makundi haijapoteza mchezo wowote wa nyumbani huku USM Alger ikiwa ni mechi ya pili kupoteza kwenye michuano hii.
Hii inakuwa ni mechi ya kwanza kwenye robo fainali.