Hatua hii inakuja baada ya uvunjifu wa usalama ulioshuhudiwa Jumatatu iliyopita kwenye mechi ya Kenya dhidi ya Morocco, ambapo idadi kubwa ya mashabiki waliingia uwanjani kuliko kiwango kilichoruhusiwa.



Mauzo ya tiketi kwa mechi hiyo yamesitishwa kwa muda na muuzaji rasmi, ikiwemo tiketi za mtandaoni ambapo CAF imesisitiza kuwa hakutakuwa na tiketi za ziada zaidi ya hizo 27,000 zilizowekwa na mashabiki wanahimizwa kufika mapema ili kuepuka msongamano.



Mechi hiyo ya hatua ya makundi itakuwa muhimu kwa Harambee Stars ambao wanatafuta ushindi muhimu dhidi ya Chipolopolo ya Zambia ili kuhakikisha wanatinga hatua ya robo fainali ya Michuano ya CHAN 2024.

You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement