Afisa Habari wa Yanga SC, Ally Kamwe ametozwa faini ya TZS milioni 1 na Bodi ya Ligi Kuu Tanzania Bara kwa kosa la kumkejeli na kumdhalilisha mwamuzi, Tatu Malogo kupitia mitandao ya kijamii.

Imeelezwa kuwa, Kamwe alichapisha picha ya mwamuzi huyo katika ukurasa wake wa Instagram akiunganisha na wimbo wa Billnas uitwao ‘Maokoto,’ hali iliyotoa tafsiri ya kumhusisha mwamuzi huyo na masuala ya rushwa.

You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement