Bondia wa Tanzania Ezra Paulo Mwanjwango anatarajiwa kupanda ulingoni usiku wa leo dhidi ya Mujinga Frazier kutoka DR Congo katika michezo ya Afrika Accra 2023 inayoendelea nchini Ghana.

Pambano hilo la robo fainali katika uzani wa Lightweight 60kg linatarajiwa kufanyika katika session ya kuanzia majira ya saa 4 usiku, muda wa Tanzania.

Ezra amefanikiwa kufika hatua hiyo ya robo fainali baada ya kushinda pambano la 16 bora siku ya Jumamosi (juzi) dhidi ya William Mohamed kutoka Shelisheli (Seychelles) katika round ya pili kwa mwamuzi kusimamisha pambano yaani RSC (Referee stop the contest)

Ushindi wa leo Ezra utamuhakikishia kucheza nusu fainali na kuingia katika mkondo wa medali kwa Taifa letu Tanzania ambalo mpaka sasa tuna uhakika wa kupata medali 1 kwenye mchezo wa ngumi kutoka kwa Cruiserweight Musa Maregesi.

You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement