Bodi ya ligi kuu Tanzania Bara (TPLB) imetangaza rasmi msimu mpya wa Ligi Kuu Tanzania Bara 2024-25 unataraji kuanza mnamo Agosti 16 huku Michuano ya NBC Championship ikipangwa kuanza kutimua vumbi Septemba 14 ya mwaka huu wa 2024.

Kwa upande wa michezo ya ufunguzi ya ligi kuu ya Soka Tanzania Bara maarufu kama michezo ya ngao ya jamii yaani Community Shield ikipangwa kuanza kuchezwa kati ya Agosti 8 mpaka 11 mwaka huu.

Taarifa ya TPLB imeeleza kuwa ligi kuu inatarajia kumalizika mnamo Mei 24 huku Michuano ya NBC Championship yenyewe ikitarajiwa kutamatika Mei 10 mwaka 2025 ambapo mchezo wa fainali ya kombe la FA utachezwa mnamo Mei 31ya mwaka 2025.

Bingwa Mtetezi wa ligi kuu Tanzania Bara msimu uliopita 2023-24 ni klabu ya Yanga SC huku timu mbili ambazo zimepanda kwa msimu huu ni pamoja na timu za Kengold FC kutoka Tukuyu Mbeya na Pamba Jiji FC kutoka Mwanza. 

You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement