Mwanariadha Mkongwe wa Jamaica na Bingwa wa zamani wa Olimpiki Usain Bolt, ameonyesha athari za jeraha alilolipata jana wakati akicheza soka katika mechi ya hisani.

Katika kipindi cha pili, Bolt aliumia na kutolewa uwanjani akiwa amebebwa kwenye machela.


Mechi hiyo iliyochezwa huko Stamford Bridge jijini London ilihusisha watu mashuhuri wakiwemo wachezaji wa zamani.

Mechi hiyo ilikuwa na lengo la kuchagia fedha za misaada kwa Shirika la Umoja wa Mataifa la watoto (UNICEF) jambo ambalo lilifanikiwa kwa kiasi kikubwa.


Baadhi ya watu waliocheza katika mechi hiyo ni pamoja na Mo Farah, Danny Dyer, Jermaine Defoe na Theo Walcott.

You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement