Mchezaji nambari moja wa zamani wa dunia na bingwa mara tano katoka mji mkuu wa Uhispania kwa upande wa Tenisi wanaume Rafael Nadal ameweka wazi kuwa imekuwa wiki ngumu kwake mara baada ya kupoteza na kutupwa nje ya mashindano Madrid Open.

Nadal mwenye umri wa miaka 37 alipungia mkono kuaga mashindano hayo baada ya kushindwa kwa seti 7-5, 6 -4 na Jiri Lehecka.

Nadal ameeleza kuwa hii Ilikuwa wiki maalum kwake iliyokuja na hisia chanya ambapo Licha ya kushindwa, mafanikio ya awali ya Nadal kwenye mashindano hayo yaliadhimishwa kwa kuonyeshwa video na kutunukiwa kombe la ukumbusho.

Umati wa watu wengi katika Uwanja wa Manolo Santana ulikata tamaa lakini mapumziko pekee yalitosha kwa Lehecka kumalizia ushindi baada ya kupata pointi yake ya kwanza baada ya saa mbili na dakika tatu.

Na sasa Lehecka tamenyana na mshindi wa tatu kutoka Urusi Daniil Medvedev, ambaye alimshinda Alexander Bublik wa Kazakhstan.

Wakati huohuo, Nadal, ambaye alirejea kutoka katika jeraha la miezi mitatu kwenye michuano ya wazi ya Barcelona mapema mwezi huu, atapata imani kutokana na ushindi wake tatu huko Madrid kwamba anaweza kushiriki michuano ya French Open kwa mara ya mwisho.

You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement