TIMU ya biashara UTD kutokea mara imepanga msimu ujao wanapanda ligi kuu kwa kuhakikisha kwamba wanawafunga timu ya Tabora united ya Tabora katika michezo yote. 

Mchezo wa kwanza ni jumatano umbao utapigwa pale CCM Karume baada ya hapo siku ya jumamosi ni pale Al Hassan Mwinyi, hivyo biashara wanahitaji matokeo mazurii. 


Kupitia mipango wanayo panga Rais wa klabu ya biashara UTD bwana Revocatus Gumila sambamba na CEO Madam Liliana pamoja na baadhi ya wabunge wa mkoa wa mara wameketi pamoja kusuka mipango namna ya kuiteketeza timu ya Tabora united 

Biashara walifanikiwa kushinda mtoano wa NBC championship league DHIDI ya Mbeya Kwanza hivyo wana matumaini makubwa sana ya kushinda kulingana na mwenendo mbaya wa Tabora united hivyo wanaamini wanaweza kupita na kufanya maajabu kama walivyo fanya Mashujaa dhidi ya Mbeya city msimu uliopita

You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement