BENZEMA KUPOKONYWA URAIA WA UFARANSA PAMOJA NA BALLON D' OR
Seneta wa Ufaransa Valerie Boyer, ameibuka na kutoa
kauli tata dhidi ya mshambuliaji huyo wa zamani wa Real Madrid.
Kupitia taarifa kwa vyombo vya habari, Seneta huyo ametaka hatua kali
zichukuliwe dhidi ya Benzema, ikiwa tuhuma za kujihusisha na kundi la "Muslim
Brotherhood" kutoka kwa Waziri wa Mambo ya Ndani zitathibitishwa.
Kwenye taarifa hiyo, Seneta Boyer alisema, "Kama kauli za Waziri wa Mambo
ya Ndani ni kweli, lazima Karim Benzema awekewe vikwazo".
"Kwanza Benzema apokonywe tuzo yake ya Ballon d'Or, lakini pia, ni lazima
mchezaji huyo avuliwe uraia wa Ufaransa. Hatuwezi kukubali Mfaransa mwenye
uraia pacha, na kujulikana kimataifa, atuvunjie heshima na kuisaliti nchi yake kwa kiasi hiki."
ijadala na tuhama hizo imeibuka baada ya Benzema kukaa kimya juu
shambulio la kigaidi lililohisisha mauaji ya mwalimu wa Kifaransa nje kidogo ya
jiji la Paris, huku siku chache baada ya tukio hilo, mchezaji huyo wa zamani wa
Real Madrid akitumia kurasa zake za kijamü, kupelekea salamu za pole na
kuomba haki itendeke kwa Taifa la Palestina.