Mechi ya ligi kuu ya soka nchini Uhispania La Liga, kati ya Valencia na Real Madrid ilimalizika kwa utata 2-2 wakati bao la Real Madrid lililofungwa na Bellingham lilipokataliwa.

Jude Bellingham alifunga kilichoonekana kuwa goli la 3 la Madrid dakika ya 99 na kuelekea ushindi wa kurudi kutoka nyuma wa 3-2.

Hata hivyo, mwamuzi alipiga kipenga kabla ya mpira kutoka nje na kumaliza mechi, na kuzua vurugu baada ya mechi.

Jude Bellingham alipewa kadi nyekundu na Mchezaji huyo wa Kimataifa wa England anakabiliwa na marufuku ya mechi mbili, na huenda akakosa mechi mbili.

Vijana wa Carlo Ancelotti walikuwa na nafasi bora ya kuwa pointi 9 mbele ya Girona, huku mbio za taji zikianza kufikia kileleni, lakini sare hiyo iliwanyima pointi tatu muhimu.

You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement