Imetaarifiwa kuwa Beki wa Kaizer Chiefs ya nchini Afrika Kusini , Luke Fleurs [24] amefariki Dunia baada ya kupigwa risasi na watu wasiojulikana.

Tukio hilo limeripotiwa kutokea usiku wa jana Johannesburg nchini Afrika kusini na kabla ya kufanyiwa tukio hilo vyanzo vinaarifu kuwa Luke alitekwa .

Vyanzo vya kiusalama nchini Afrika kusini kupitia kwa Msemaji wa polisi wa Gauteng, Lt-Kanali Mavela Masondo alisema bado hajapokea ripoti rasmi kuhusu tukio hilo.

Meneja wa mawasiliano wa kampuni ya Chiefs, Vina Maphosa alisema klabu hiyo bado haiwezi kuzungumzia suala hilo.

Fleurs alijiunga na Kaizer Chiefs kama mchezaji huru mwezi Oktoba baada ya kuachana na klabu ya awali ya SuperSport United mwezi Septemba mwaka jana.

Fleurs ameitumikia SuperSport michezo 70, ambayo alijiunga nayo kutoka daraja la kwanza Ubuntu FC mnamo mwaka 2018.

You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement