MICHEZO ya wikiendi hii itachezeshwa na VAR Kwa Mkapa, CAF imeweka bayana marefa wa wasaidizi watakaosimamia VAR, ambapo Dahane Beida kutoka Mauritania atasimamia shoo hiyo ya Simba.

Beida atasaidiwa na Ahmad Imtehaz kutoka Mauritius katika mechi kati ya Simba na Al Ahly leo saa 3:00 usiku Kwa Mkapa, jijini Dar es Salaam.

Beida mwenye umri wa miaka 32, ni miongoni mwa waamuzi vijana wanaofanya vizuri kwa sasa na hii sio mara yake ya kwanza kuchezesha mechi iliyokutanisha vigogo hawa, kwani alikuwa ndio mwamuzi wa kati kwenye mechi ya ufunguzi ya Simba na Ahly katika African Football League.



You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement