Kama wewe ni shabiki wa Arsenal na ulitarajia itakuwa kazi rahisi kuindoa Bayern kutokana na kiwango kibovu kilichoonyeshwa na Bayern msimu huu kwenye ligi ya Bundesliga basi inapaswa ufikilia tena.

Mshambuliaji wa Bayern, Harry Kane (30) amesema Bayern Munich wamelazimika kuwekeza nguvu zao kwenye ligi ya UEFA baada ya kuporomoka kwao na kuzima matumaini ya kutetea taji lao la Bundesliga kufuatia kiwango kibovu walichoonyesha msimu huu kwenye ligi hiyo.

Bayern wamepoteza michezo yao miwili ya mwisho ya Bundesliga na kuiacha Bayer Leverkusen ikielekea ukingoni mwa taji lao la kwanza kabisa. Miamba hao wa Bavaria wameshinda taji la Ujerumani kwa miaka 11 iliyopita na Kane alikiri kiwango chao cha ligi kimeweka shinikizo zaidi kwao kufanikiwa Ulaya.



You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement