Bayern Munich inataka kuanza mazungumzo na Manchester City kwa ajili ya kuipata saini ya winga wa timu hiyo na Ureno, Bernardo Silva, 29, ambaye mkataba wake unaweza ukavunjwa ikiwa timu inayomhitaji itatoa Pauni 50 milioni.

Kwa muda mrefu Silva amekuwa akitajwa kwamba anataka kuondoka kwa ajili ya kutafuta changamoto mpya sehemu nyingine.

Awali, Silva alikuwa akihusishwa na Barcelona lakini ni ngumu timu hiyo kumpata kwa sababu haina uwezo wa kutoa kiasi cha pesa ambacho kinahitajika ili kumnunua.

Mbali ya Barcelona, Man United pia ilikuwa ikihusishwa naye lakini inaonekana kuwa ngumu kutokana na upinzani uliopo baina ya timu hiyo na Man City.

Mkataba wa sasa wa fundi huyu wa kimataifa wa Ureno unatarajiwa kumalizika mwaka 2026. Msimu uliopita alicheza mechi 51 za michuano yote, akafunga mabao 12 na kutoa asisti 10.

Hivi sasa Silva anawasha moto kwenye fainali za Mataifa ya Ulaya (Euro).

You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement