BAYERN Munich imemtangaza Vincent Kompany kuwa kocha wao mkuu akitua Allianz Arena kuchukua mikoba ya Thomas Tuchel.

Bayern imeamua kuachana na Mjerumani Tuchel baada ya kuambulia patupu kwenye Bundesliga msimu wa 2023/2024, ilipomaliza nafasi ya tatu kwenye msimamo huku ikiishia pia kwenye nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Hata hivyo, Bayern imeamua kumpa kazi Kompany, ambaye ametoka kuishusha daraja timu ya Burnley kwenye Ligi Kuu England, ambapo msimu ujao itakuwa kwenye Championship.

Mkataba wake Mbelgiji Kompany huko Allianz Arena utafika ukomo 2027.

Akizungumza katika utambulisho wake, Kompany amesema: " Ni heshima kubwa kupewa nafasi hii, nitafanya kazi vizuri na kila mtu kwenye timu kutengeneza kitu kizuri ambacho mashabiki watapenda kuona au kusikia kuhusu klabu yao."

You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement