Shangwe la ubingwa wa Ligi Kuu Bara kwa Yanga msimu huu linaendelea kukaribia baada ya ushindi ilioupata wa bao 1-0, dhidi ya Mashajaa katika mchezo mkali na wa kusisimua uliopigwa kwenye Uwanja wa Lake Tanganyika mkoani Kigoma.

Bao pekee na la ushindi kwa Yanga limefungwa na nyota mshambuliaji wa timu hiyo, Joseph Guede dakika ya 41 ya kipindi cha kwanza baada ya kupiga shuti lililomshinda kipa wa Mashujaa, Patrick Munthar akiunganisha krosi ya, Mudathir Yahya.

Guede aliyejiunga na timu hiyo dirisha dogo la Januari mwaka huu akitoke Klabu ya Tuzlaspor ya Uturuki, ameendeleza kiwango bora akiwa na kikosi hicho kwani bao la leo ni la tano kwake katika Ligi Kuu Bara hadi sasa kwa msimu huu.

Ushindi huu unaifanya Yanga kufikisha pointi 65 katika michezo 25 iliyocheza hivyo kuhitaji pointi nane tu ili kufikisha 73 zitakazowapa ubingwa wa Ligi Kuu Bara kwa mara ya tatu mfululizo na ya 30 kwa ujumla kwani hazitaweza kufikiwa na timu yoyote.




You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement