Mchezaji wa timu ya Miami Heat ligi kuu ya mpira wa kikapu nchini marekani Bam Adebayor ameandika historia Alfajiri ya Leo akisaidia timu yake kupata ushindi wa point 109 - 108 Lakers ya Lebron James , Kwenye mechi hio Adebayor amefunga point 22 , Assist 10 na Rebound 20.

Wiki hii Bam Adebayor amechaguliwa kuwa captain wa Miami Heat na amefanikiwa kuandika historia ya kuwa mchezaji wa kwanza kwenye historia ya Miami Heat kufunga point 20+ , kutoa Assist 10+ na kuchukua Rebound 20+ Kwenye game Moja ya NBA. 

Bam Adebayor amefanikiwa kuandika historia hio ikiwa Lebron James amewahi kucheza Miami Heat na amewahi kuchukua ubingwa mala mbili katika miaka minne ambayo amecheza na timu hio na ajawahi kufikia rekodi ambayo Bam Adebayor ameweka.

You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement