MAKIPA wawili wa Azam FC, AbdulaiIddrisu na Ali Ahamada wameondolewa kwenye usajili wa kikosi hicho baada yakuonekana watakuwa nje ya uwanja kwa muda mrefu kutokana nakusumbuliwa na majeraha mbalimbali waliyoyapata mwaka jana.

Iddrisu anauguza jeraha la bega lake lamkono wa kushoto alilofanyiwaupasuaji nchini Afrika Kusini sambamba na Ahamada anayesumbuliwa na goti la mguu wakushoto huku akiondoka na kwendaUfaransa kwa ajili ya uchunguzi wamatibabu zaidi.

Makipa hao wote ambao wamekuwa nichaguo la kwanza watakaa nje yauwanja kwa takribani miezi minne hadi mitano hivyo viongozi kushtuka nakuwaondoa kwenye usajili ili kupisha nyota wengine wapya waliosajiliwa dirisha hii kuongeza nguvu.

Mastaa wapya waliosajiliwa na kikosihicho ni kipa, Mohamed Mustafa aliyetokea Al-Merrikh ya Sudan, beki wakati, Yeison Fuentes aliyetoka timu ya Leones FC na mshambuliaji, Franklin Navarro aliyesajiliwa kutoka Cortulua FC ya kwao Colombia.

Mbali na kuondolewa mnastaa hao, timuhiyo ilitangaza kuachana na aliyekuwamshambuliaji, Idris Mbombo aliyetuaNkana ya Zambia.

You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement