Mchezo wa Ligi Kuu Bara kati ya Azam FC na Mashujaa umemalizika kwenye Uwanja wa Azam Complex Chamazi Kwa timu hizo kutoka suluhu.

Azam iliingia katika mchezo huu ikiwa na kumbukumbu nzuri ya ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Namungo huku kwa upande wa Mashujaa ikitoka kuchapwa 2-1 mbele ya Coastal Union.

Katika mchezo wa mzunguko wa kwanza baina ya timu hizo uliopigwa kwenye Uwanja wa Lake Tanganyika Kigoma, Azam ilishinda mabao 3-0.

Kwa matokeo haya yanaifanya Azam kufikisha jumla ya michezo 23 ambapo kati ya hiyo imeshinda 15, sare sita na kupoteza miwili ikiendelea kusalia nafasi ya pili na pointi 51.

Kwa upande wa Mashujaa katika michezo yao 23 iliyocheza, imeshinda mitano tu, sare saba na kupoteza 11 ikiendelea kusalia nafasi ya 15 na pointi 22.

Matokeo mengine ya michezo ya leo, Geita Gold ililazimishwa suluhu na Maafande wa Tanzania Prisons kwenye Uwanja wa Nyankumbu Geita huku Tabora United ikichapwa mabao 3-0 na Kagera Sugar kwenye Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi Tabora.

Kwenye Uwanja wa Majaliwa mkoani Lindi, wenyeji Namungo iliyochapwa na Azam FC mabao 2-0, mechi iliyopita ilizinduka leo na kuifunga Coastal Union bao 1-0, lililofungwa na nyota wa timu hiyo, Hassan Kabunda dakika ya nane.







You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement