Klabu za Simba, Azam na Yanga SC zimeendelea na maandalizi sambamba na maboresho ya vikosi kwajili ya msimu ujao w amashindano.

Kwa upande wa Klabu ya Simba wao wameshawasili nchini Misri katika mji wa Ismailia ambapo wameanza mazoezi huku wakitangaza rasmi kuachana na kiungo wa Kimataifa wa Mali, Sadio Kanoute.

Kwa upande wa Klabu ya Yanga wao wamemtambulisha rasmi kiungo Mzambia, Clatous Chota Chama huku kikosi hicho kikiendelea na mazoezi kuelekea msimu mpya wa mshindano.

Klabu ya Azam FC wao wameelekea Visiwani Zanzibar kwaajili ya kambi ya wiki moja kabla ya kurejea jijini Dar es salaam kwaajili ya maandalizi ya safari kuelekea Nchini Morocco kwaajili ya kambi ya muda mrefu.

Mkuu wa kitengo cha Habari Azam FC Thabith Zakaria ameweka wazi kuwa wameondoka na kikosi chote kwa maana ya wachezaji ambao wanahitajika tiba sambamba na wazima na kuongeza pia juu ya sajili au utambulisho wa wachezaji wapya ndani ya Klabu hiyo.

You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement