Azam FC imetangaza kuanza kurejea kambini Julai Mosi hadi nne rasmi kwa ajili ya maandalizi ya msimu mpya wa 2024/25.

Meneja wa habari na mawasiliano wa klabu hiyo Thabit Zakaria (Zakazakazi) amesema timu hiyo itaanza kupokea wachezaji kuanzia Julai Mosi hadi nne ambapo rasmi kikosi hicho kitafanya mazoezi Julai tano hadi sita kwenye Uwanja wa Azam Complex.

Ameongeza kuwa kikosi hicho kitasafiri kwenda Zanzibar kwa kambi ya siku sita kuanzia Julai sita hadi 13 ambapo kitarudi Dar es Salaam na rasmi Julai 14 kikosi kitaelekea Morocco kwenye kambi ndefu hadi mwishoni mwa mwezi.


Zaka amesema tayari kikosi hicho kimeshaachana na wachezaji wake watano ambao ni Issah Ndala, Malckou Ndoye, Edward Manyama, Daniel Amoah na Ayoub Lyanga lakini sio mwisho kwani lolote linaweza kutokea katika dirisha hili la usajili.

Ameongeza kuwa kikosi hicho kwenye msimu wa 2024/25, kitajikita zaidi kwenye kuwania ubingwa kwenye mashindano watakayoshikiri kwani kutwaa ubingwa ndio itakuwa furaha yao.

Azam FC msimu ujao itashiriki mashindano ya Ligi ya Mabingwa Afrika, Ligi Kuu, FA, Ngao ya Jamii na Kombe la Mapinduzi.

Hadi sasa Azam FC imetambulisha wachezaji watano wanne wa nje na mmoja wa ndani.

You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement