Shirikisho la soka la Australia litaanzisha uchunguzi wa kumuacha nyota Nestory Irankunda baada ya timu hiyo kushindwa kufuzu michuano ya Olimpiki yatakayofanyika mwaka huu. 

Australia haikufunga hata goli moja wakati wa mechi zake zote za makundi baada ya kumuacha Irankunda nje. 

Irankunda alijizoelea umaarufu baada ya kupachika mabao 11 katika mechi 7 akikiwakilisha kikosi cha U17 cha timu ya Taifa ya Australia. 

Akiwa ni mtoto wanne kati ya saba, Irankunda alizaliwa katika kambi ya wakimbizi nchini Tanzania, kabla ya familia yake kuhamia Australia alipokuwa na umri wa miezi mitatu tu.

Kabla ya hapo, wazazi wake walikimbia vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini Burundi na kupokelewa kwenye kambi ya wakimbizi mkoani Kigoma, nchini Tanzania.

You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement