Klabu ya Simba imethibitisha kuwa kwenye kilele cha Wiki ya Simba Day itakayozinduliwa kuanzia Julai 29 mpaka Agosti 6, 2023, Wekundu hao wa Msimbazi watacheza mechi ya kirafiki dhidi ya Mabingwa wa Ligi Kuu Zambia 2022/23, klabu ya Power Dynamos

Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari, meneja wa habari wa klabu hiyo Ahmed Ally amebainisha kuwa viingilio Vingilio vya Simba Day vitakuwa kama ifuatavyo:-

Platinum Tsh. 200,000,

VIP A - Tsh. 40,000,

VIP B Tsh. 30,000,

VIP C Tsh. 20000,

Machungwa - Tsh. 10,000 na

Mzunguko Tsh. 5,000.

“Kwa upande wa vingilio, sisi kama klabu tunahitaji fedha lakini kwenye tamasha tunahitaji zaidi mashabiki, Wanasimba waje zaidi ndio maana tunawatafuta wadhamini kama CRDB ili walete fedha. Tunajali zaidi maslahi ya Wanasimba.” amesema 

“Kispika kinarudi mtaani kuwaita Wanasimba kwenye Simba Day. Tunaenda kuwaonyesha kwamba Uwanja wa Mkapa ni mdogo sana kwa Simba kuujaza.”

“Waliopandisha kibegi kwenye Mlima Kilimanajaro, watu wote tisa tutawaalika kwenye Simba Day na watapata nafasi ya kutambuliwa na mashabiki kwenye siku ya tamasha letu."

"Kikosi kitarejea kutoka Uturuki tarehe 1 ya mwezi Agosti."- Ahmed Ally.

You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement