Mechi nyingine za marudiano Robo Fainali UEFA Europa League, AS Roma imeichapa AC Milan bao 2-1 na inasonga mbele kwa ushindi wa jumla wa bao 3-1 baada ya kushinda 1-0 kwenye mechi ya kwanza.

Nayo Bayer Leverkusen imelazimisha sare ya bao 1-1 na wenyeji West Ham United na hivyo Leverkusen inasonga mbele kwa ushindi wa jumla wa bao 3-1 kufuatia kushinda bao 2-0 kwenye mechi ya kwanza nyumbani.

Nao Marseille wameitoa Benfica kwa penalti 4-2 kufuatia sare ya jumla ya 2-2, wakifungwa 2-1 Ureno kwenye mechi ya kwanza wiki iliyopita kabla ya kushinda 1-0 katika mchezo wa marudiano nchini Ufaransa.

Katika Nusu Fainali za UEFA Europa League, Marseille itamenyana na Atalanta na Roma dhidi ya Bayer Leverkusen na mechi za kwanza zitafanyika Mei 2 na zile za marudiano zikipigwa Mei 9 ambapo Marseille na Roma wataanzia nyumbani.

You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement