Arsenal imejiandaa kupokea ofa na kumuuza mshambuliaji wao raia wa Brazil, Gabriel Jesus katika dirisha lijalo la majira ya kiangazi.

Jesus mwenye umri wa miaka 27 anaripotiwa kuwa kwenye mpango wa kuuzwa na Arsenal kutokana na majeraha yake ya mara kwa mara yanayosababisha awe nje ya uwanja kwa muda mrefu.

Msimu huu Jesus amecheza mechi 24 za michuano yote na kufunga mabao manne na haonekani kuwa kipaumbele kwa kocha Mikel Arteta kutokana na kukosa takwimu zenye kushawishi hasa za ufungaji wa mabao akifunikwa na Kai Havertz.

Nafasi yake muda mwingi huwa anacheza Kai Havertz ambaye tangu kuanza kwa msimu huu ndio anaonekana kuaminika zaidi na Arteta.

Tangu Januari mwaka huu, Jesus amecheza mechi 13 tu za michuano yote na kati ya hizo ni tatu tu ndio alianza kwenye kikosi cha kwanza na zilizobakia aliingia akitokea benchini.

Bado ana mkataba hadi mwaka 2027 lakini haonekani kumvutia tena Arteta, hivyo Arsenal inafikiria kumuuza na kutumia pesa itakazopata kwa ajili ya kuboresha zaidi timu hiyo.






You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement