Arsenal imeambiwa kwamba kama kweli ipo siriazi kwenye mpango wa kunasa saini ya kiungo wa Aston Villa, Douglas Luiz, basi itatakiwa kulipa mkwanja unaoanzia Pauni 50 milioni kwenda juu.

Kiungo huyo wa Kibrazili alikuwa na wakati mzuri kwenye kikosi hicho cha Villa Park kwa msimu uliopita na kuwasaidia kukamatia tiketi ya kucheza Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu ujao. Alifunga mabao 10 na kuasisti 10.

Aston Villa iliwahi kugomea ofa ya kumpiga bei Luiz huko nyuma, lakini sasa ipo tayari kufanya biashara kwenye dirisha hili la uhamisho wa majira ya kiangazi ili kuweka sawa vitabu vyake vya hesabu ili kwenda sawa na ishu ya mapato na matumizi. Klabu zote zenye uwiano usiokuwa sawa kwenye matumizi na mapato zitahitaji kuuza wachezaji wake kabla ya kufika siku ya mwisho ya Juni 30.

Na hilo linaweza kumlazimisha kocha wa Aston Villa, Unai Emery kukubali kuuza silaha yake hiyo muhimu kabisa kwa wapinzani wao Arsenal, ambao kwa muda mrefu wamekuwa wakimfukuzia Luiz. Na kwenye hilo, Aston Villa imeweka wazi kiasi cha pesa inachohitaji kwenye mauzo ya kiungo huyo. Luiz alijiunga na Aston Villa kwa ada ya Pauni 15 milioni kutokea Manchester City mwaka 2019.

Arsenal iliwahi kushuhudia ofa yao ya Pauni 25 milioni ya kumtaka mchezaji huyo ikikataliwa mwaka 2022. Juventus na AC Milan nazo zinatoa macho kuhitaji huduma ya mchezaji. Na sasa Aston Villa imeanza mazungumza na kiungo wa Chelsea, Conor Gallagher ili kuja kurithi mikoba ya Luiz, wakiamini watampata kwa gharama ya chini kiasi. Villa wao wanamuuza Luiz kwa Pauni 50 milioni.

You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement