Mara baada ya kumalizana na Kocha Raia wa Ujerumani Jürgen Norbert Klopp na kumtambulisha Arne Slot kuwa Kocha wa Klabu ya Liverpool, Slot ameeleza kuwa ilikuwa ni ngumu kuikataa fursa ya kufanya kazi katika mojawapo ya klabu kubwa zaidi duniani ilikuwa "ngumu kuipuuza.

Klopp, ambaye alikuwa akiinoa Liverpool tangu Oktoba 2015, aliondoka katika klabu hiyo kufuatia ushindi wao wa fainali ya msimu dhidi ya Wolves Jumapili.

Mkataba wa Slot wa miaka mitatu ndani ya Liverpool unatajwa kuanza rasmi Juni Mosi mwaka huu, chini ya kibali cha kufanya kazi.

Mholanzi huyo alichukua nafasi ya ukocha ndani ya Klabu ya Feyenoord mnamo mwaka 2021 na aliiongoza Feyenoord kutwaa taji la Eredivisie 2022-23, wakati msimu huu wameshinda Kombe la Uholanzi na kumaliza nafasi ya pili kwenye ligi ambapo alithibitisha nia yake ya kusimamia Ligi ya Premia alipohusishwa na Tottenham mnamo 2023.

Kufuatia tangazo la Liverpool siku ya Jumatatu ya Mei 20, Mohamed Salah alionekana kupendekeza kuwa atasalia Anfield msimu ujao.

Liverpool ilikataa ofa ya pauni milioni 150 kutoka kwa Al-Ittihad kwa ajili ya Salah msimu uliopita wa joto, lakini mkurugenzi wa soka wa Saudi Pro League Michael Emenalo baadaye alisema mlango haujafungwa kwa winga huyo wa Misri.

You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement