Winga wa zamani wa Real Madrid na Manchester United, Angel Di Maria ametangaza kustaafu soka la kimataifa kwa mafanikio makubwa kwa taifa lake la Argentina baada ya miaka 16.

Nyota huyo akiwa na Argentina kwa miaka minne wamefanikiwa kushinda mataji manne ikiwemo Kombe la Dunia, Copa America mara 2 pamoja Finalissima 2022.

Di Maria (36) ameshiriki katika Fainali nne za Kombe la Dunia (2010, 2014, 2018, na 2022), na kufika fainali huko Brazil 2014 na kisha 2022 kufanikiwa kushinda Kombe hilo huko Qatar.

Katika michuano ya Copa America, mzaliwa huyo wa Rosario alishiriki katika fainali mfululizo (2015 na 2016), dhidi ya Chile mara zote mbili na kutoka patupu na hatimaye mwaka 2021 alifanikiwa kunyanyua taji hilo akifunga bao muhimu dhidi ya Brazil kwenye Uwanja wa MaracanĂ£, kisha mwaka huu amebeba tena.

Argentina ndiyo mabingwa wa muda wote wa Copa America ikiwa imechukua taji hilo mara 16, ikifuatiwa na Uruguay mara 15 huku Brazil ikiwa imebeba mara tisa.

You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement