ALMAS KASONGO ASHANGAZWA NA TABIA ZA MASHABIKI WA TIMU PAMOJA NA WACHEZAJI WAO KUWA NA TABIA ZA KISHIRIKINA
Mtendaji mkuu wa Bodi ya Ligi, Almas Kasongo ameshangazwa na tabia za baadhi ya mashabiki na wachezaji wanapoona mambo yanakuwa magumu kwenye timu zao wanakuwa na taswira kichwani na kuamua kuingia uwanjani kutoa taulo za makipa wakati mechi ikiwa inaendelea.
Kasongo amesema tabia hizo ni uvunjifu wa kanuni kwa sababu hazimhitaji mtu yeyote ndani ya uwanja isipokuwa wale ambao wametajwa kikanuni ambao wanapaswa kuwepo kwenye eneo la ufundi.
Ameongeza kuwa kuwepo kwa mwendelezo wa tabia hizo wana mashaka na walinzi ambao wanahusika na usalama ambapo vilabu wanalitumia ndivyo sivyo kutokana na kanuni mpya ambayo shughuli ya huduma wa mchezo kwa sasa zipo kwenye klabu mwenyeji ambapo amekasimiwa madaraka ya kuhudumia mchezo wake.
Hata hivyo amesema hatua kali zitachukuliwa kwa yeyote aliyehusika au atakayehusika na vitendo hivyo ili kulinda thamani ya Ligi.