Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Yanga, Ally Kamwe amezungumzia hali ya majeruhi waliopo katika klabu hiyo kuelekea mchezo wa robo fainali Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Mamelodi utakaochezwa Machi 30, 2024.

Akizungumza na waandishi wa habari leo, Kamwe amesema beki Yao Kouassi yupo hatarini kuukosa mchezo huo kutokana na kuchanika kwa nyama za paja.

“Kibwana Shomari anaendelea vizuri na ataanza mazoezi hivi karibuni.”

“Khalid Aucho yeye anaendelea na sehemu ya pili ya matibabu.”

Ameongeza kuwa, Pacome Zouzoua anaendelea na matibabu akiwa kwenye timu ya Taifa ya Ivory Coast iliyoko kambini nchini Ufaransa.

You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement