Kuelekea katika mchezo wa Debry utakaowakutanisha watani wa Jadi utakaowakutanisha Yanga SC dhidi ya Simba SC, Uongozi wa Klabu ya Yanga umeweka wazi kuwa japo wapinzani wao wamekuwa na matokeo yasiyoridhisha lakini wanaamini bado wanakikosi kizuri.

Mkuu wa Kitengo cha Habari Yanga SC Ally Kamwe amesema kuwa kwa sasa wanachopitia Simba SC ni mapito na wanaamini ubovu wao utakuja mara baada ya Aprili 20.

Kikosi cha Simba SC leo kinatarajia kuelekea Visiwani Zanzibar kwaajili ya kambi ya maandalizi ya mchezo wao dhidi ya Yanga utakaopigwa Aprili 20 katika Dimba la Mkapa jijini Dar es salaam.

Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano Simba Ahmed Ally ameeleza kuwa wanaamini kambi hiyo itajenga utulivu kwa wachezaji wanaokabiliwa na ratiba ngumu ya Ligi.

You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement