AL Ahly watatua kwenye ardhi ya Tanzania leo kuikabili Yanga Jumamosi jioni. Lakini kiungo wao,Aliou Dieng amekiri kwamba wako kwenye presha kubwa kuelekea mchezo huo.

Amekiri kwamba wamepata fursa ya kuipekua Yanga haswa kwenye mechi ya mwisho dhidi ya CR Belouizdad lakini wamegundua ina mabadiliko makubwa kiuchezaji, lakini kinachowaumiza ni kukosa matokeo kila wanapokanyaga kwa mkapa Dieng ambaye ni panga pangua, alisema bado wanajitafuta kwa jinsi gani watapata matokeo ya ushindi kwenye ardhi ya Tanzania kwasasa kwani tangu ametua Ahly hajashinda Kwa Mkapa na mara ya mwisho walisare katika mechi ambayo waliamini watashinda.

"Tulipokuja Tanzania mara ya mwisho kucheza na Simba tuliona kwamba ni mchezo ambayo tulistahili kushinda kwa jinsi tulivyoianza mechi lakini baadaye tukafanya makosa ya kuruhusu mabao mawili ya haraka," alisema Dieng.

"Tunakuja tukijua kwamba tunakwenda kucheza uwanja mgumu kwasasa kwetu tunataka kuhakikisha kwamba tunabadilisha haya matokeo ingawa tunajua tunakwenda kukutana na timu nyingine ngumu," alisema Dieng na kukiri kuwa Yanga ina wachezaji bora ambapo amekuwa akipata taarifa nyingi za ubora wao kwa kumfuatilia kipa wa timu hiyo Djigui Diarra ambaye ni rafiki yake.

"Ukiangalia Diarra ni kipa mzuri na mkubwa wapo wachezaji wengine lakini kubwa ni hii kucheza fainali ya shirikisho msimu uliopita kwahiyo tunawaheshimu lakini tutapambana nao kutafuta alama tatu." Ahly mara ya mwisho kuja nchini ilikuwa ni Oktoba 20 walipocheza dhidi ya Simba mchezo ambao licha ya Waarabu hao kuanza kwa kasi kwa kutangulia kupata bao lakini wekundu hao walisawazisha kisha kupata bao la pili na mchezo kumalizika kwa sare ya mabao 2-2.

Ahly wamewahi kupoteza mara moja mbele ya Yanga kwenye mechi zao 10 ilikuwa Machi mosi 2014 kwa bao 1-1 ambapo baadaye walikutana tena Aprili 9,2016 na kutoka sare ya bao 1-1. Waarabu hao pia wakapoteza mara mbili dhidi ya Simba kwa miaka miwili tofauti matokeo kabla ya kupata sare.

You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement