Mtibwa Sugar imemtambulisha Zuberi Katwila kurejea kwenye klabu hiyo kama Kocha Mkuu kufuatia kuachana na Habib Kondo aliyeoiongoza timu kwenye mechi tano tu ikiambulia pointi mbili.

Mechi iliyopita Mtibwa Sugar ikifungwa 2-1 na Kagera Sugar Uwanja wa Manungu Complex, Turiani mkoani Morogoro timu iliongozwa na makocha Wasaidizi, Awadh Juma na Patrick Mwangata.

Katwila anajiunga tena na Mtibwa Sugar akitokea Ihefu SC ambako aliiongoza timu katika mechi tano za msimu pia ikivuna pointi sita, kabla ya kuokota pointi ya saba juzi katika sare ya 0-0 na Coastal UniĆ³n Uwanja wa Highland Estate, Mbarali mkoani Mbeya.

You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement