Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Yanga, Ali Kamwe amesema wanachokitaka sasa kwenye mashindano ya Ligi ya Mabingwa Afrika ni kufika fainali na sio robo.

Akizungumza na waandishi wa habari leo, Kamwe amesema japokuwa wamefuzu robo fainali, bado wanataka kuifunga Al Ahly kwao ili kuweka rekodi mpya na kutinga hatua ya robo fainali Yanga ikiongoza kundi D.

Amesema hakuna timu yeyote wanayoihofia bali wanaziheshimu tu kwani wanaamini katika ubora wao.

“Timu yoyote hata Mamelodi Sundowns waletwe tu maana hakuna timu tunayoihofia ila tunaiheshimu tu kwani tunaamini ubora wao."

You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement