Takriban mwaka mmoja baada ya kuanza kwa vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini Sudan, klabu yenye mafanikio makubwa zaidi ya soka nchini humo, Al Hilal, inasema inaendelea kucheza ili kutoa " bughudha" kwa watu nchini Sudan.

Mzozo huo umesababisha vifo vya zaidi ya watu 14,000 na kuwalazimu watu milioni 8 kuyakimbia makazi yao na Umoja wa Mataifa umeonya kuwa huenda ukasababisha mzozo mkubwa zaidi wa chakula duniani.

Michuano ya taifa ilikatizwa lakini mabingwa hao wa Sudan walipata mwanya wa kuendelea na shughuli zao uwanjani kwa kufikia makubaliano na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kucheza na timu zake kuanzia Agosti.

"Tunacheza wakati huu wa mzozo ili kundoka fikra za watu wetu kutoka kwenye vita," Dk Hassan Ali, katibu mkuu wa Al Hilal.

“Wengi wa mashabiki wa soka nchini Sudan wakati mwingine hawana lolote hata katika nyakati za kawaida, walichonacho ni ushindi wa Al Hilal ambao unawafanya wawe na furaha na familia zao.

"Ni jukumu la kimaadili. Sio kucheza ili kushinda alama au vikombe. Hapana, tunacheza kwa ajili ya wafuasi wetu ili kuweka ari yao."

Klabu hii ya takribani karne moja, inayoshiriki Ligi ya Mabingwa Afrika, ilituma maombi kwa mashirikisho mengine kadhaa barani kote na kupokea majibu chanya kutoka Uganda na Libya kabla ya kufanya makubaliano na Tanzania.

"Tulipendelea Tanzania kwa sababu mpira wa miguu huko ni wa maendeleo na wenye ushindani, na tungependa kujiandaa vyema kwa mashindano yajayo katika ngazi ya Afrika," aliongeza Dk Ali.

Kuifahamu Tanzania pia kulichangia, kwani Tanzania ndiyo iliyokuwa tegemeo la klabu hiyo wakati wa kampeni za Ligi ya Mabingwa msimu huu ambazo zilimalizika kwa kuondolewa katika hatua ya makundi.

Msemaji wa TFF , nchini Tanzania, Clifford Mario Ndimbo aliambia BBC kwamba vilabu vyote kwenye ligi vinaunga mkono kujumuishwa kwa Al Hilal, lakini mechi zao zitahesabiwa kuwa za kirafiki.

Kucheza nchini Tanzania kunaweza pia kuisaidia Al Hilal kuepuka kuhama kwa wachezaji wengi kabla ya ushiriki wao katika mashindano ya bara msimu ujao.

Klabu hiyo yenye maskani yake Omdurman kwa sasa ina takribani wachezaji kumi wa kigeni katika kikosi chake.

"Nadhani itawasaidia Al Hilal kuwabakisha wachezaji wao na Florent Ibenge, kocha ambaye anajulikana katika bara zima na ana jukumu kubwa katika kile wanachojaribu kufanya," mchambuzi wa soka wa Sudan Abdul Musa alisema.

"Wanahitaji aina fulani ya ushindani ambao wanaweza kuwa tayari kushindana katika ngazi ya bara. Ikiwa hutacheza ligi, ni vigumu."

You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement