Simba imeishia Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika mara ya nne katika misimu sita baada ya kupokea kichapo cha jumla ya mabao 3-0 na Al Ahly bingwa mtetezi wa michuano hiyo.

Simba imepoteza ugenini mabao 2-0 Cairo yakifungwa Amr El Solia dakika ya 47 na Mahmoud Kahraba kwa penalti dakika ya 90 huku bao la kwanza lilifungwa na Ahmed Nabil Koka Machi 29, katika Uwanja wa Mkapa.

Ahly anasikilizia mshindi kati ya TP Mazembe dhidi ya Atlético Petróleos de Luanda itayopigwa leo Aprili 6 katika Uwanja wa 11 de Novembro, Angola saa 1:00 usiku.



You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement