Zikiwa zimebaki siku nne tu kabla ya SIMBA kuvaana na Al Ahly katika mechi ya uzinduzi wa Ligi mpya ya Afrika ‘African Football League’, Kocha Roberto Oliveira ‘Robertinho’ ameweka wazi kuanza kwa Golikipa Aishi Manula

Kocha Robertinho katika mahojiano na gazeti la Mwanaspoti amethibitisha kuridhishwa na kiwango cha Manula na moja kwa moja ameamua kumuweka kwenye mipango ya mchezo huo wa Ijumaa “Kila kocha anatamani kuwa na wachezaji wote kikosini, tumefurahi kumwona Manula akirejea lakini kwa kuonyesha kiwango bora. Kitu kizuri amerejea wakati tukijiandaa na mechi ya Al Ahly, ni mchezaji mzoefu na tayari tumemjumuisha kwenye mipango yangu kama ilivyo kwa wengine,”

You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement