AISHA MASAKA KUTINGA UEFA CHAMPIONS AKIWA NA BK HACKEN YA SWEDEN
Aisha Masaka baada ya chama lake, BK Hacken la Sweden kutinga hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa ya Wanawake ya Ulaya na litakutana na Real Madrid (W) pamoja na Chelsea (W).
BK Hacken imetinga hatua hiyo baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 kwenye mchezo wa mkondo wa pili ugenini huko Uholanzi ambako ilikuwa ikimalizana na wenyeji wake, Twente na kwenye mchezo wa kwanza ilitoka sare ya mabao 2-2. Ushindi wa jumla ya mabao 3-2, umelifanya chama hilo la Masaka kutinga hatua ya makundi ambayo imepangwa sambamba na vigogo wawili kwenye soka la Ulaya upande wa wanawake, Chelsea ya England na Real Madrid ya Hispania.
Akizungumzia kitendo cha kupangwa kundi moja na vigogo hao, Masaka amesema ni fursa ambayo alikuwa akitamani kuipata kwani kucheza dhidi ya Chelsea, Real Madrid na hata Paris FC ya Ufaransa si jambo dogo. "Moja kati ya ndoto yangu ni kucheza kwenye ligi kubwa zaidi Ulaya, hivyo kwenda England, Hispania na Ufaransa ni fursa ya kuonyesha kipaji changu maana mashindano haya yanafuatiliwa na klabu nyingi, nina imani Uefa itanifungulia milango ya kupiga hatua zaidi" anasema na kuongeza.
Haikuwa kazi nyepesi kwetu kuingia hatua ya makundi, mchezo wa kwanza tulitoka sare nyumbani, tulikuwa na kazi ngumu na kubwa ya kufanya ugenini lakini jambo zuri ni mpango wetu ambao tulienda nao Uholanzi ulifanikiwa na ndoto sasa zimetimia za kucheza hatua ya makundi ya ligi ya mabingwa." Kocha wa BK Hacken,
Mak Lind amewapongeza wachezaji wake kwa kazi kubwa ambayo waliifanya Uholanzi hadi kutinga hatua ya makundi huku ikishuhudiwa Manchester United, VfL Wolfsburg zikitupwa nje.
amewapongeza wachezaji wake kwa kazi kubwa ambayo walifanya Uholanzi hadi kutinga hatua ya malkundi huku ikishuhudiwa Manchester United, VfL
Wolfsburg zikitupwa nje. "Shabaha yetu kwa sasa ni kufanya vizuri pia kwenye hatua ya makundi, tutajiandaa na yoyote ambaye atakuwa mbele yetu," anasema kocha huyo. Hizi ni dondoo muhimu za wapinzani wa BK Hacken ambayo anaichezea Masaka.