Baadhi ya Mashabiki wa Simba waliojilipia nauli zao kusafiri kwenda kuipa sapoti timu yao Nchini Misri.

Kila shabiki amejilipia Dola 1200 sawa na Milioni 3,126,000

Hili swala la Serikali kusafirisha Mashabiki nitatoa maoni yangu nikimalizana na Al Ahly, Sasa hivi akili inawaza namna ya kufuzu Nusu Fainali, Ila msimamo wangu ni kwamba si jambo jema hata kidogo.

Kwa Mashabiki mpira ni starehe hivyo Serikali haiwezi kugharamia watu kwenda kustarehe, Tena bora ingekua imetoa usafiri tu. Lakini wametoa Posho Dola 500 kila kichwa sawa na Milioni 1,200,000 kwa ufupi hawa Mashabiki wamenuniliwa na wanalipwa kuishangilia timu yao.

Na hao sio Mashabiki wa kawaida ni Machawa wanaotetea maslahi ya viongozi wao yaani Serikali imelipia Machawa wa watu,Kuwalipia nauli sio kuwapenda ni kufuga tatizo ambalo baadae hatutaweza kulitatua.

Leo unalipia mashabiki wa klabu, kesho Ali Kiba ataiomba Serikali iwagharamie mashabiki wake kwenda Marekani kufanya show utamnyima??

Twaha Kiduku ataomba aende kupigana Uingereza na mashabiki wake utamnyima??

Halafu nyie Nyuma Mwiko acheni kuzuga huwezi kulipia nauli watu 48 ukajidai eti unawapenda mashabiki zenu, Wakati kwenye mechi yenu juzi Mashabiki wameumia, wamepigwa mabomu ya machozi, watu wamepata vilema, na hamjasema chochote halafu uje uzuge eti unawapenda watu wenu.

Ndugu zangu wana Simba hili swala lisiwatie unyonge na wala Serikali yetu haina nia ya kufanya ubaguzi, Sisi tuendelee na utamaduni wetu kujisimamia tukipata msaada tutachukua lakini katu tusilemae kusubiri dezo

We are Simba Sisi ni Wakubwa, Sisi ni Wafalme, Sisi tuna hadhi kubwa.

You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement